Friday, March 31, 2023
  • About Us
  • Contact Us
Parliamentobserver
  • Ecology
  • Economy
  • Healthcare
  • Politics
  • Education
  • Business
  • Login
No Result
View All Result
Parliamentobserver
Home Ecology

Na Eve Davidian: Hadithi ya mapenzi, msongo na kinyesi cha fisi Ngorongoro

Dennis Rogers by Dennis Rogers
September 29, 2022
in Ecology
0
Na Eve Davidian: Hadithi ya mapenzi, msongo na kinyesi cha fisi Ngorongoro
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

An English version of this blogpost is available here.

Kuna pengo la kiuelewa kuhusu uhusiano kati ya cheo cha mwanaume kijamii na mafanikio yake katika uzazi. Hii ni kwa mujibu wa utafiti nilioufanya na mwenzangu, miongoni mwa wanyama. Utafiti huu unaonyesha kuwa mfumo wa kijamii na kujamiiana wa fisi wenye madoadoa unaweza kutoa mwanga katika kuelewa mienendo ya usawa wa uzazi miongoni mwa jamii za mamalia.

Related posts

Using functional traits to identify conservation priorities for the world’s crocodylians: Podcast transcript

September 29, 2022
Awheto: the new gold?

Awheto: the new gold?

September 29, 2022

Katika jamii nyingi za wanyama, rasilimali hazigawiwi kwa usawa miongoni mwa kikundi. Wale walio katika ngazi ya juu ya uongozi wa kijamii hula chakula kitamu zaidi, hupata sehemu za kulala zenye starehe, na wanaweza kupata wenzi wanaovutia zaidi.

Katika ulimwengu wa wanyama, ambapo mafanikio ya maisha huamuliwa kwa kiasi kikubwa na idadi ya watoto ambao mnyama huacha nyuma, ni wazi kwa nini bidii hufanyika ili kufikia kilele na kubaki huko kwa muda mrefu iwezekanavyo.

Jambo ambalo bado hatuelewi kabisa ni jinsi cheo cha kijamii kinavyoathiri mafanikio ya uzazi. Je, madume wa vyeo vya juu huzaa watoto zaidi na watoto wenye ubora wa juu kwa sababu wana nguvu na kuvutia zaidi? Au ni kwa sababu hawana wasiwasi wowote kwenye ushindani na madume wengine na wana uwezo wa kuwapata majike zaidi?

Ili kujibu maswali haya, tulifanya utafiti nyikani katika savanna ya Kiafrika. Kwa zaidi ya miaka 20 – na karibu miezi 20 ya Shahada yangu ya Uzamivu tulijikita katika kutafuta, kutambua, kutathmini uzao, na kufuatilia tabia ya maelfu ya fisi walio na madoadoa kutoka kwa koo nane za utafiti katika Bonde la Ngorongoro Kaskazini mwa Tanzania.

Pia ia tulikusanya zaidi ya vinyesi 400 vya fisi ili kupima mkusanyiko wa vichocheo vya cortisol na kukadiria, kifisiolojia, kuwa fisi hao wanapata mfadhaiko au msongo wa mawazo kiasi gani. 

Tulipata ushahidi wa wazi kwamba mwingiliano na madume wengine huwa na mfadhaiko zaidi kwa madume wa vyeo vya chini kuliko wapinzani wao wa vyeo vya juu na kwamba hii inaathiri nguvu wanazoweza kuwekeza katika kuwachumbia majike waliojaaliwa na wanaoshindaniwa zaidi.

Pia tuligundua kuwa madume wanapaswa kuchanganua mapenzi na majukumu ya kawaida zaidi kama kufahamiana na wenzi wapya wa koo na kudumisha urafiki wa zamani na ushirikiano wa kimkakati. Lakini madume wa vyeo vya chini huepuka shughuli zenye kuwasababishia msongo wa mawazo na kutumia muda zaidi wakiwa peke yao, kumeza mifupa au kutulia kwenye madimbwi yenye uvundo.

Madume wa ngazi ya juu, kwa upande mwingine, wanahitaji muda mdogo wao kuwa wenyewe ili kuondoa msongo, na wanaweza kuwekeza mengi zaidi katika kukuza uhusiano wa kirafiki na majike. Na hilo ndilo jambo ambalo fisi jike hupenda zaidi.

Katika jamii ya fisi wenye madoadoa, mapenzi kwa kiasi kikubwa yanaamriwa na kile ambacho majike wanataka. Kinyume na madume wa mamalia wengine wengi fisi dume hawawezi kuwalazimisha kingono majike kwa sababu sehemu za siri za kike zimebadilishwa kiume kuwa kifaa chakuzuia ubakaji. Njia pekee iliyopo nikuwa rafiki: Picha na Oliver Höner

Pia, tuligundua falsafa za madume wale ambao hupendelea kukaa nyumbani au wale “wavulana wa mama” –hawa hutoa kipaumbele kwa maswala ya uzazi badala ya kukuza mahusiano ya kijamii, na kuzingatia juhudi zao za uzazi kwa majike wenye ubora wa juu – matokeo yake hujikuta wakiwa katika  nafasi ya juu kijamii ikilinganishwa  na wahamiaji.

Awali, tuligundua kuwa madume wa falsafa huzaliana mapema kuliko wahamiaji na kuzaa watoto karibu na majike wa daraja la juu pekee na matokeo yasasa yanaweza kulingamishwa na hayo ya awali katika kuelewa jinsi wanaume wanavyotofautiana.

Tofauti na spishi nyingi ambapo madume hutumia nguvu zao za kimwili, pembe ndefu na meno makali ili kuwazuia wapinzani – au hata kuwalazimisha ngono majike – fisi dume wenye madoadoa hawashiriki katika mapigano makali ili kufika kileleni mwa uongozi na kuzaliana. Kwa nini basi madume  wa vyeo vya chini wana msongo wa mawazo zaidi kuliko madume wa vyeo vya juu?

Fisi dume wanaweza wasiwe wanyama wakali lakini pia si wanyama wenye kupenda amani. Katika utafiti wa hivi karibuni tulionyesha kuwa uhusiano wa kiukutawala katika jamii ya fisi kimsingi hutegemea ni washirika wangapi wa kijamii ambao fisi anaweza kutegemea anapokuwa katika mzozo na wengine.

Madume wa ngazi ya chini kwa kawaida ni wageni na hawana ushirikiano wenye nguvu. Pia wako hatarini zaidi kutumiwa na wengine kama mbuzi wa kafara na hii inaweza kuwa chanzo kikuu msongo wa mawazo au mfadhaiko.

Unyanyasaji hutokea mara kwa mara miongoni mwa fisi (na wanyama wengine) na inaelekea hutumika kama njia ya kupunguza msongo au kukabiliana na mafadhaiko kisaikolojia.

Mara nyingi fisi huchukua mfumo wa msururu wa utawala ambapo madume yanayofuatana huelekeza tena uchokozi hadi kwa dume mwingine wa ngazi ya chini. Na wakati dume wa cheo cha chini kabisa kwenye mnyororo kama huo hana mnyonge wake, kukimbilia kwa mbweha asiye na hatia, mwamba, au hata gari letu la utafiti.

Lakini usiwaonee huruma madume wa chini. Wakati wao utafika.

Cheo cha kijamii cha fisi dume wenye madoadoa huamuliwa na mkusanyiko wa kupanga foleni. Madume wengi hatimaye hupanda ngazi ya kijamii na kupata kufurahia manufaa ya kuwa katika nafasi ya juu kijamii.

Inafurahisha sana kuona kwamba hata katika jamii ambapo mahusiano ya utawala yanarasimishwa na mifumo yakijamii, mwingiliano kati ya madume unaweza kuwa na athari kifiziolojia kitu ambacho kinaweza kushinikiza marekebisho ya kitabia yenye athdari (ya gharama) kiuzazi.

Utafiti wetu unarekebisha uelewa wetu kuhusu jinsi cheo cha kijamii kinavyohusiana na msongo wa mawazo na jinsi ushindani wa wanaume unavyoathiri fiziolojia, ujamaa na uimara. Pia unatoa mtazamo mpya juu ya utaratibu wakifisiolojia unaoweza kuibua mikakati mbadala ya uzazi na kuzaliana.

Makala haya yametafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza na Deusdedity Masemba, kwaajili ya kuchapishwa katika gazeti la ‘MwanaSayansi’. MwanaSayansi ni gazeti la kwanza la Sayansi kwa Kiswahili nchini Tanzania na chanzo mahususi cha habari, maoni & uchambuzi kuhusu sayansi & teknolojia.

Dr. Eve Davidian, mwandishi wa kwanza alikamilisha utafiti, huu kama sehemu ya Shahada yake ya Uzamivu, pamoja na Dr. Oliver Höner na Prof. Heribert Hofer kutoka Chuo Kiku cha Freie Universität na Taasisi ya Leibniz ya Zoo- na Wanyamapori huko Berlin (Ujerumani). 

Previous Post

Eve Davidian: Why do the top dogs get the prettiest ladies? A story of sex, stress and hyena poops

Next Post

The Panic Reveals So Much: Elon Musk, Twitter, and the Digital Public Sphere

Next Post
The Panic Reveals So Much: Elon Musk, Twitter, and the Digital Public Sphere

The Panic Reveals So Much: Elon Musk, Twitter, and the Digital Public Sphere

RECOMMENDED NEWS

Review: The Great Experiment by Yasha Mounck

Review: The Great Experiment by Yasha Mounck

9 months ago
How the Fed Painted Us into a Corner

How the Fed Painted Us into a Corner

1 year ago
The California primary—what happened to the revolution?

The California primary—what happened to the revolution?

10 months ago
What’s behind the globalization of R&D?

What’s behind the globalization of R&D?

1 year ago

BROWSE BY CATEGORIES

  • Business
  • Ecology
  • Economy
  • Education
  • Healthcare
  • Politics

POPULAR NEWS

  • Klaus Schwab – The Most Dangerous Man in the World

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Dr. Robert Malone v WEF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Ukraine Adopts WEF Proposals

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Trudeau’s Approval Rating Hits 12-Month Low

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • Trudeau Backs Down After Banks Scream about Massive Withdrawals

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
Parliamentobserver

We bring you latest news about ecology, economy, healthcare, politics, education, business.

Recent News

  • Supporting Ukrainian Economy: #SpendWithUkraine Initiative Launched by Ukrainian Brands
  • Starting Up: A Look at the Most Interesting Websites for Entrepreneurs and Startups
  • The Role of Healthcare Advertising in Shaping Economic and Political Decisions

Category

  • Business
  • Ecology
  • Economy
  • Education
  • Healthcare
  • Politics

Recent News

Supporting Ukrainian Economy: #SpendWithUkraine Initiative Launched by Ukrainian Brands

Supporting Ukrainian Economy: #SpendWithUkraine Initiative Launched by Ukrainian Brands

February 6, 2023
Starting Up: A Look at the Most Interesting Websites for Entrepreneurs and Startups

Starting Up: A Look at the Most Interesting Websites for Entrepreneurs and Startups

January 18, 2023
  • About Us
  • Contact Us

© 2022 parliamentobserver.com Submit news release

No Result
View All Result
  • Ecology
  • Economy
  • Healthcare
  • Politics
  • Education
  • Business

© 2022 parliamentobserver.com Submit news release

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In